nitazidi kuongea
kwa sababu nikiongea
mababu wangu huongea
wale washupavu walionitangulia
zile sauti zilizoshindwa kuongea
wazalendo wangu wanaongea
jamii yangu inaongea
wale niliowajua na wale sikuwajua
wale ambao ninaweza kuwafikiria
lakini cha mhimu
roho yangu inaongea
utu wangu unaongea
ndoto zangu zinaongea
sifa yangu inaongea
mambo mengi sana
kwa hivyo nitaendelea kuongea
nitazidi kuongea
No comments:
Post a Comment